Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefafanua kurejea nchini kwa kiraka Erasto Nyoni ambaye alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa kule Cameroon
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo imebainisha kuwa Nyoni amelazimika kurejeshwa nyumbani ili kuendelea na matibabu majeraha aliyopata baada ya ushauri wa madaktari wa timu
Tangu alipotua Cameroon, Nyoni alishindwa kufanya mazoezi na timu kutokana na majeraha hayo
"Mchezaji Erasto Nyoni amepewa ruhusa ya kuondoka kwenye kambi ya Taifa Stars, amerudi nyumbani kuendelea na matibabu baada ya kushauriwa na jopo la Madaktari wa timu," ilisema taarifa ya TFF

ADVERTISE HERE