Djuma asema Gendarmerie wepesi, ushindi mnono tena

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Feb 2018
Djuma asema Gendarmerie wepesi, ushindi mnono tena
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba, wanamatumaini makubwa ya kutinga kwa kishindo hatua inayofuata ya michuano hiyo na tayari wameanza kuwapigia hesabu Waarabu wa Misri, Al Masry.

Simba iliondoka jana majira saa 11 jioni kuelekea Djibouti kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Gendamarie ya nchini humo huku Wekundu wa Msimbazi hao wakiwa na hazina kubwa ya mabao 4-0 waliyoyapata katika mechi ya awali kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema wameenda Djibouti wakiwa na matumaini ya ushindi kutokana na maandalizi yao na namna walivyo na uchu wa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

"Sisi tuko vizuri kuelekea kwenye mchezo wetu wa marudiano, tunaenda kwa dhamira ya kupata ushindi, tena ikiwezekana ushindi mkubwa kuliko ule tulioupata hapa Dar es Salaam," alisema Djuma.

Alisema tayari wameanza kupiga mahesabu ya mchezo unaofuata baada ya hatua hii ya awali ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na 'waarabu' wa Al Masry ya Misri ambao nao wapo mbele kwa mabao 4-0 waliyoyapata dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

"Tumepania Simba kufanya vizuri kwenye michuano hii ya Afrika, kila mchezo kwetu tunauchukulia kama fainali, tumewaelekeza wachezaji wetu kutumia vyema kila nafasi nzuri ya kufunga..., na kwa umakini wa wachezaji tunauhakika wa kufanya hivyo," alisema Djuma.

Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kurejea kwa mshambuliaji wao, John Bocco, ambaye aliumia na kulazimika kutoka nje kwenye mchezo wa Ligi Kuu Alhamisi iliyopita dhidi ya Mwadui FC.

Bocco, amejumuishwa kwenye msafara wa wachezaji 20 walioelekea Djibouti jana kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’