Sasa ni rasmi, uongozi wa klabu ya Simba umemtangaza Didier Gomez Da Rossa kuwa kocha mkuu wa mabingwa hao wa nchi
Gomez alitua nchini mapema leo akitokea Sudan baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Al Marreikh ambayo iko kundi moja na Simba ligi ya mabingwa hatua ya makundi
Gomez amesaini mkataba wa miaka miwili mbele ya Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez katika tukio lililofanyika Serena Hotel mapema leo
Gomez ameeleza furaha yake kujiunga Simba akiahidi kufanya kazi kwa weledi
Mtaalam huyo amepewa jukumu la kutinga nusu fainali michuano ya ligi ya mabingwa, kutetea ubingwa wa ligi kuu na kombe la FA
Sasa kazi na ianze...!
ADVERTISE HERE