Mshambuliaji wa Simba raia wa Burundi, Laudit Mavugo, amekiri kuwa bado hajawa kwenye kiwango chake cha juu tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mavugo ameachwa kwenye msafara wa wachezaji waliokwenda Djibouti kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gendarmerie.
Akizungumzia mwenendo wake usioridhisha msimu huu, Mavugo amesema hali hiyo inaweza kumtokea mchezaji yeyote lakini anachokifanya sasa ni kuhakikisha anarejesha makali yake.
"Unajua huu ni mpira..., na mambo haya hutokea kwa mchezaji yoyote, ni kweli sijawa kwenye kiwango changu, lakini naendelea kupambana na naamini nitakuwa sawa hivi karibuni," alisema Mavugo.
"Naendelea kupambana na kufuata maelekezo ya makocha..., mimi ni mchezaji na najiamini, mashabiki wa Simba wasiwe na hofu na mimi, nitawafurahisha tu," aliongeza kusema Mavugo.
Mavugo pia amezungumzia ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi cha Simba.
"Hii inasaidia kuleta ushindani ndani ya timu, Simba inawachezaji wengi wenye uwezo mkubwa, hivyo nina uhakika msimu huu itafanya vizuri," alisema Mavugo.
Katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui, Mavugo aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya John Bocco, lakini hata hivyo, alijikuta akitolewa tena kabla ya mchezo kumalizika kutokana na kiwango cha chini alichokionyesha.

ADVERTISE HERE