Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa michuano ya CHAN inayoendelea Cameroon kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo itashuka dimbani kutupa karata yake ya pili dhidi ya Namibia
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa nne usiku ukitanguliwa na mchezo kati ya Uganda dhidi ya Guinea
Tanzania inahitaji matokeo ya ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbela hatua ya mtoano ya michuani hiyo
Kocha Etienne Ndayiragije amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo na leo wameahidi kupambana kuhakikisha wanashinda
Kama Tanzania itafungwa leo basi itakuwa imeyaaga rasmi mashindano hayo
Dua za Watanzania wazalendo ni kwa kikosi chetu leo kiweze kupata matokeo mazuri ili tusonge mbele
ADVERTISE HERE