Klabu ya Simba imetambulisha mashindano maalum yatakayofahamika kama Simba Inter Cup yatakayohusisha vilabu vitatu Simba, TP Mazembe na Al Hilal kutoka Sudan
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema michuano hiyo itaanza Januari 27 na itamalizika Januari 31
Simba itatumia michuano kama sehemu ya maandalizi ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mbaingwa
Aidha mabingwa hao wa nchi watatambulisha wachezaji wapya waliowaongeza katika kipindi cha dirisha dogo
Kuhusu ujio wa kocha mkuu, kosho Jumamosi Simba itamtangaza kocha huyo pamoja na wasaidizi wake wawili
"Tunatangaza mashindano mapya ya SIMBA INTER CUP ambayo yatashirikisha timu tatu. Simba SC, TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan. Mashindano yataanza Januari 27 hadi 31, 2021," alisema Barbara
"Kupitia mashindano haya Wanasimba watapata nafasi ya kuwaona wachezaji wapya na kocha. Kuanzia kesho tutatangaza watu ambao tumewaongeza katika benchi la ufundi."