Baadae leo uongozi wa klabu ya Simba utakuwa na Mkutano na Wanahabari Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam
Mkutano huo utafanyika kuanzia saa nane mchana
Matarajio ya wengi ni kuwa kupitia Mkutano huo, Simba itamtambulisha rasmi kocha wake Mkuu ambaye Jumatatu ataanza majukumu ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa nchi kuelekea mechi za ligi ya mabingwa pamoja na ligi kuu
Inafahamika Simba ilifanya mazungumzo na kocha wa AS Vita na timu ya Taifa ya DR Congo Florente Ibenge wakati alipokuja nchini na timu yake ya Taifa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania
Je ni yeye? Tusubiri saa nane pale viongozi watakapozungumza na wanahabari
ADVERTISE HERE