Katika mchezo wa kwanza michuano ya CHAN dhidi ya Zambia, nafasi ya ulinzi wa kushoto alianza Edward Charles Manyama nyota wa zamani wa Namungo Fc ambao katika usajili wa dirisha dogo amejiunga na Ruvu Shooting
Lakini ni wazi, Manyama alifanya majukumu ya ulinzi tu, hakuwa akiipandisha timu pengine hofu ya kushiriki michuano mikubwa kwa mara ya kwanza ilichangia
Ni wazi benchi la ufundi sasa wanaweza kuona jinsi gani walifanya makosa kumuacha beki wa Simba Mohammed Hussein 'Tshabalala'
Tshabalala amekuwa beki tegemeo wa Stars upande wa kushoto kwa karibu miaka minne sasa
Ana uzoefu wa kutosha katika kushiriki michuano ya Kimataifa, kacheza makundi ligi ya mabingwa lakini pia alishiriki michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika Misri
Katika kikosi alichoteua kocha Etienne Ndayiragije nyota wengi alioenda nao Cameroon wamekosa uzoefu
Hii inaweza kuwa sababu Stars ikaondolewa mapema kwenye michuano hiyo