Klabu ya Simba ilikamilisha kwa wakati usajili wa kiungo Mcongomani Doxa Gikanji ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa nchi kwa ajili ya ligi kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa
Jina la Gikanji ni miongoni mwa majina ya wachezaji 10 wa kigeni waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya VPL baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa
Nyota huyo amechukua nafasi ya Taddeo Lwanga ambaye atabaki na majukumu ya ligi ya mabingwa tu
Gikanji anatua Simba akitokea klabu ya DC Motema Pembe ya DR Congo
Ni kiungo fundi anayemudu vyema majukumu ya nafasi zote za kiungo cha kati, sasa yuko kule Cameroon na kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo
Gikanji na Perfect Chikwende wameongezwa katika kikosi kitakachoshiriki VPL ambapo Chikwende amechukua nafasi ya Francis Kahata ambaye pia anabaki na jukumu la Ligi ya Mabingwa tu