Nkamia aahidi umoja, mshikamano Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Jan 2021
Nkamia aahidi umoja, mshikamano Simba

Mgombea wa nafasi ya mwenyekiti ndani ya klabu ya Simba, Juma Nkamia amesema moja ya kipaumbele chake kama atachaguliwa atahakikikisha anashirikiana na wanachama nchi nzima kuwapa uhuru wa kuchangia mawazo kwa ajili ya maendeleo ya timu.

Nkamia ambaye alikuwa Mbunge wa Chemba, Dodoma, yupo kwenye kinyang'anyiro hicho na Martaza Mangungu ambaye naye alikuwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Swedi Nkwabi katika uchaguzi mdogo uliopangwa kufanyika Februari 7, mwaka huu

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nkamia alisema sio mgeni ndani ya klabu hiyo kwani alishawahi kuwa katibu mwenezi wa Simba, hivyo anafahamu matamanio na maono ya wanachama wa timu hiyo

"Niwaombe wapenzi na wanachama kunipa fursa ya kunichagua siku ya uchaguzi, pamoja na kuwa na vipaumbele vinne ambavyo naamini vimekuwa vikiwasumbua Simba"

"Nitawaunganisha wanachama nchi nzima na kuwapa fursa ya kutoa mchango wa mawazo kwa maendeleo ya timu" alisema Nkamia aliyewahi pia kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Alisema vipaumbele vingine ni kusimamia mabadiliko ambayo mchakato wake umeshaanza kufanyika kwa kushirikiana vyema na Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, kutatua baadhi ya changamoto ikiwamo kinachoendelea dhidi ya tume ya ushindani (FCC) kwa kufanya kikao cha pamoja kumaliza tofauti

Pia alisema kwakuwa mchezo wa soka unahitaji uwekezaji mkubwa, akipewa ridhaa hiyo atashirikiana na viongozi wengine kuongeza vyanzo vingine vya mapato kwa maslahi ya timu

Alisema kampeni zake anatarajia kuzindua keshokutwa jijini Dar es Salaam na baada ya hapo atafanya kikao na waandishi wa habari kabla ya kutangaza ratiba ya kwenda mikoa mingine.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba, Boniface Lihamwike ametoa wito kwa wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya kampeni ya wagombea ili kuwapima na sera zao waweze kuchagua kiongozi bora

"Wanachama wasibeze na kususia kampeni wajitokeze kwa wingi kuwapima wagombea kwani tumetoa kipindi kikubwa cha wagombea kupita kujinadi kuomba kura wapate fursa ya kuchaguliwa" alisema.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
19h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’