Baada ya kukosa takribani mechi saba akisimamishwa na uongozi wa Simba kutokana na utovu wa nidhamu, kiungo fundi Jonas Mkude 'Nungunungu' anatarajiwa kurejeshwa kikosini karibuni
Kamati ya Nidhamu ya klabu Simba tayari imekutana na kukubaliana kuwa Mkude asipewe adhabu zaidi baada ya kusimamishwa kwa zaidi ya wiki tatu
"Mkude atarejeshwa kikosini timu itakapoanza maandalizi ya mechi za ligi ya mabingwa. Hakutakuwa na adhabu zaidi ya muda ambao tayari amekaa nje ya kikosi, pengine atapigwa faini, " alisema Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Nidhamu
Simba inarejea mazoezini kesho Ijumaa kuanza maandalizi ya ligi kuu na michuano ya ligi ya mabingwa, Februari 13 wakitarajiwa kusafiri DR Congo kuikabili AS Vita
Β
ADVERTISE HERE