Kahata azungumzia hatma yake Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jan 2021
Kahata azungumzia hatma yake Simba

Kiungo Mkenya Francis Kahata amesema yeye ni mchezaji halali wa klabu ya Simba mkataba wake ukimalizika mwishoni mwa msimu

Kumekuwa na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na uongozi wa Simba kuwa Kahata hatawatumikia mabingwa hao wa nchi kwenye ligi kwa kuwa jina lake limeondolewa kumpisha kiungo mpya raia wa Zimbabwe Perfect Chikwende

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya Kahata kugomea kupelekwa kwa mkopo klabu ya Azam Fc

Kahata aliibuka kuwa mchezaji bora wa michuano ya kombe la Mapinduzi, mwenyewe amesema ataendelea kuitumikia Simba mpaka pale mkataba wake utakapomalizika

"Mambo mengi yanazungumzwa lakini nikwambie, mimi bado ni mchezaji wa Simba, nina mkataba hivyo nitaendelea kuwa hapa," alisema Kahata

Mkenya huyo alikuwa na wakati mgumu kupata namba kwenye kikosi cha kwanza wakati mabingwa hao wa nchi wakinolewa na Sven Vandenbroeck

Lakini aling'gara kule visiwani Zanzibar kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kikosi kikiwa chini ya Selemani Matola

Kahata aliibuka mchezaji bora wa mashindano na kuondoka na kitita cha Tsh Milioni nne

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’