Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amethibitisha kuwa nahodha John Bocco atakosekana katika mchezo wa kwanza wa fainali za michuano ya CHAN dhidi ya Zambia
Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo ambao utapigwa saa moja usiku, Ndayiragije amesema Bocco bado hajapona sawasawa majeraha aliyopata katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Fc Platinum
Hata hivyo amesema wachezaji wengine wako tayari kwa mchezo huo, anaamini watawashangaza wengi
"Timu yangu ipo vizuri na Itawashagaza watu wengi kwenye mashindano haya, Siiogopi Zambia kwa sababu nawajua Vizuri wachezaji wa Zambia na hata ligi yao,Pia namfahamu Vizuri kocha wao "
"Licha ya kumkosa Mshambuliaji John Bocco ambaye alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika lakini nina Wachezaji wengine wa kucheza nafasi yake"
"Timu yangu ina Wachezaji wengi wadogo na wageni kwenye mashindano makubwa ambao wapo tayari kupambana na kutetea Taifa lao," amesema