Simba kuongeza wawili ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Jan 2021
Simba kuongeza wawili ligi ya mabingwa

Dhamira ya Simba msimu huu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ni kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ambayo hatua ya makundi inaanza mwezi ujao

Mabingwa hao wa nchi wanaendelea kuboresha kikosi chao kwa ajili ya michuano hiyo ikielezwa kuwa wako mbioni kukamilisha usajili wa nyota wengine wawili wa Kimataifa

Kiungo Mcongomani Karim Ntikubuka anatajwa kuwa usajili unaosubiri kukamilishwa na mabosi hao wa Msimbazi

Nyota huyu mwenye umri wa miaka 19 anaitumikia klabu ya DC Motema Pembe kutoka DR Congo na yuko kwenye kikosi cha DR Congo kinachoshiriki michuano ya CHAN kule Cameroon

Miamba hao wa soka nchini pia wanaweza kumsajili beki Peter Muduhwa kutoka Highlanders Zimbabwe ambaye pia yuko kwenye kikosi cha Zimbabwe kinachoshiriki michuano ya CHAN

Simba imepanga kuongeza nyota watano wa kigeni kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake cha michuano ligi ya mabingwa

Mabingwa hao wa nchi tayari wameinasa saini ya mshambuliaji wa zamani wa Esperance, Junior Lokosa kutoka Nigeria huku pia wakimsajili Perfect Chikwende kutoka Platinum Fc

Hata hivyo Chikwende hataweza kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa inayoendelea kulingana na kanuni za CAF kwa kuwa tayari ameitumikia Platinum Fc katika michuano hiyo

Nyota huyo ameongezwa katika kikosi cha ligi kuu akitajwa kuchukua nafasi ya Francis Kahata anayesubiri mkataba wake umalizike mwezi Juni

Kahata ataendelea kuitumikia Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’