Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Etienne Ndayiragije amesema wanakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Zambia michuano ya CHAN hapo kesho Jumanne lakini wako tayari kuwakabili mabingwa hao wa zamani Afrika
Kesho Januari 19 2021 majira ya saa moja usiku kwa saa za Tanzania, katika mji wa Limbe huko Cameroon, Stars itachuana na Zambia katika mchezo wake wa kwanza kundi D
Ndayiragije amesema baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tatu nchini Cameroon, kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo
"Nashukuru tulifika salama hapa Cameroon, tunaendelea na maandalizi yetu vizuri, hali ya hewa hapa ni nzuri, tunashukuru kila kitu kipo sawa"
"Tunafahamu hatutakuwa na mchezo rahisi dhidi ya Zambia lakini jambo muhimu kwetu ni kuhakikisha tunaanza vyema michuano hii. Malengo yetu ni kufika mbali, hivyo tumewaandaa wachezaji kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huu wa kwanza," alisema Etienne
Stars iliongezewa nguvu jana baada ya kutua kocha msaidizi Selemani Matola na kiraka Erasto Nyoni ambaye awali hakusafiri na timu kutokana na matatizo ya kifamilia
Kimahesabu Tanzania inahitaji kushinda mchezo mmoja na angalau kutoka sare mchezo mmoja ili kuweza kuvuka hatua ya makundi ya michuano hiyo ambayo Stars inashiriki kwa mara ya pili
Mwaka 2009 wakati kikosi hicho kikinolewa na kocha Marcio Maximo, kilifanikiwa kutinga fainali za michuano hiyo kwa mara ya kwanza lakini walitolewa katika hatua ya makundi
Ratiba ya mechi za wiki hii
