Simba imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa na FCC kuhusu uchunguzi wa mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' amesema kuwa hawana shaka na hatua za mchakato wao hata kama FCC wameamua kufanya uchunguzi
Try Again amesema Simba ilipeleka mchakato huo FCC kwa ajili ya kuomba ushauri tu
"Sioni kama kuna tatizo lolote lililofanywa kinyume na taratibu za mfumo wa mabadiliko"
"Kikubwa wanachama tulikubaliana kuingia kwenye mfumo huu na kwao tulienda kuomba ushauri tu"
"Hivyo tunaamini kila kitu kitakwenda sawa kwani hatujakiuka taratibu zozote za mfumo huu," alisema Try Again
Juzi kupitia magazeti ya Serikali, Tume ya ushindani (FCC) ilichapisha taarifa ya kuanza uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji klabu ya Simba