Nimekuja kufanya kazi Simba - Chikwende

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jan 2021
Nimekuja kufanya kazi Simba - Chikwende

Nyota mpya wa Simba Perfect Chikwende amesema ujio wake ndani ya mabingwa hao wa nchi utakuwa wa manufaa

Kiungo huyo mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka klabu ya Fc Platinum ambayo hivi karibuni iliondoshwa na Simba katika hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa, amesema Simba ni klabu kubwa barani Afrika hivyo atahakikisha anapambana ili mchango wake uweze kuisaidia timu kutimiza malengo yake

Kuhusu ushindani wa namba, Chikwende amesema amejiunga na timu bora hivyo ushindani haliepukiki lakini muhimu kwake ni kuhakikisha anajituma kulishawishi benchi la ufundi aweze kuaminiwa

"Ni heshima kubwa kwangu kusajiliwa na Simba Sc, moja ya timu bora barani Afrika. Nimekuja hapa huku nikifahamu hii ni klabu kubwa naahidi kujituma kwa uwezo wangu wote ili kuisaidia timu kufikia malengo yake," alisema

Usajili wa Chikwende umewafurahisha wanachama na mashabiki wa Simba ambao wanaamini ujio wake utazidi kuimarisha safu ya ushambuliaji kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi inayoanza wiki ijayo

Chikwende pia amesajiliwa kushiriki ligi ya ndani ikielezwa amechukua nafasi ya Francis Kahata ambaye atabakia kwenye kikosi cha ligi ya mabingwa mpaka mwishoni mwa msimu mkataba wake utakapomalizika

Inaelezwa Simba pia imemsajili mshambuliaji raia wa Nigeria Junior Lokosa kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa

Simba inaruhusiwa kuongeza nyota watano (nje ya wale 10) wa kigeni kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’