Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Selemani Matola na beki kiraka Erasto Nyoni wameondoka nchini leo kwenda Cameroon kuungana na timu ya Taifa inayoshiriki michuano ya CHAN
Matola alikuwa na majukumu ya klabu kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuondoka aliyekuwa kocha mkuu Sven Vandenbroeck
Aidha, Nyoni alishindwa kuondoka na kikosi cha Stars kilichosafiri juzi kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia

Stars itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya CHAN keshokutwa Jumanne kwa mchezo dhidi ya Zambia
Nyoni ataiongezea nguvu safu ya ulinzi ya kikosi cha kocha Etienne Ndayiragije ambacho michuano ya mwaka huu kimepania kuvuka hatua ya makundi
ADVERTISE HERE