Morrison awaibua mashabiki Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Jan 2021
Morrison awaibua mashabiki Simba

Kutotumika kwa mshambuliaji Barnard Morrison kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, kumeibua maswali miongoni mwa mashabiki wa klabu ya Simba

Morrison alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichokuwa visiwani Zanzibara kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi iliyomalizika jana kwa Yanga kuibuka mabingwa kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Machamponi wa nchi, Simba

Morrison hakupata nafasi ya kucheza mchezo wowote na kuacha maswali kulikoni Mghana huyo hakupewa nafasi?

Katika Mkutano wake wa mwisho na wanahabari kabla ya mchezo dhidi ya Yanga, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Selemani Matola alisema kuwa Morrison alikuwa majeruhi na ndio maana hakuweza kutumika katika michezo ya nyuma

Wanamsimbazi waliamini kwa umuhimu wa mchezo wa jana, Morrison angeweza kupewa nafasi ya kuanza na pengine hata kuingia kipindi cha pili kwani mchezo ulihitaji mchezaji wa aina yake ambaye anaweza kulazimisha walinzi kufanya makosa

Safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa ikicheza mchezo wa kimabavu sana na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuwadhibiti washambuliaji walioanza, Miraji, Dilunga na Meddie Kagere kabla ya kuingia Mugalu ambaye aliongeza uhai

Morrison ni mshambuliaji mwenye kasi, skills na uwezo binafsi. Kwa aina ya mchezo ambao mabeki wa Yanga walikuwa wakicheza, Morrison angeweza kuwasababishia matatizo makubwa sana ambayo yangeinufaisha Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’