Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Selemani Matoka amesema anakiamini kikosi chake kilichotinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar
Na kuwa vijana wake wataikabili Yanga baadae leo kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo ambao utapigwa saa mbili na robo usiku uwanja wa Amaan
Tangu jana jioni kumekuwa na tetesi kuwa Simba imewaongeza kikosini wachezaji Luis Miquissone, Larry Bwalya na Clatous Chama kwa ajili ya mchezo huo
Matola amesisitiza kuwa atawatumia vijana wake alioshiriki nao tangu mchezo wa kwanza, kwani anaamini wanao uwezo wa kushinda mchezo huo na kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi kwa mara ya tano
"Wachezaji wangu wote wako tayari kwa ajili ya mchezo. Kwa wachezaji ambao hatukonao kambini itakuwa ngumu kuingia kwenye kikosi cha kwanza kwenye mechi yetu dhidi ya Yanga. Mchezo utakuwa mgumu ila tupo tayari kwa ushindani," alisema Matola