Tunautaka ubingwa Mapinduzi Cup - Matola

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Jan 2021
Tunautaka ubingwa Mapinduzi Cup - Matola

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Selemani Matola amesema kikosi chake kiko kamili kuelekea mchezo wa fainali michuano ya kombe la Mapinduzi dhidi ya watani zao Yanga ambao utapigwa baadae leo Jumatano uwanja wa Amaan

Matola amesema pamoja na mchezo huu kuwa wa dabi ambao unazikutanisha timu zenye ushindani wa asili, hilo halitawazuia kutimiza azma yao ya kuwa mabingwa wa michuano hiyo

"Hii ni fainali na hii ni Dabi, mechi itakuwa ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kutwaa ubingwa wa Mapinduzi," amesema Matola

Matola alikabidhiwa mikoba ya kuinoa Simba baada ya aliyekuwa kocha mkuu Sven Vandenbroeck kutimkia Morocco kujiunga na FAR Rabbat

Michuano ya Mapinduzi ni ya kwanza kwake akiwa kocha mkuu, na amefanikiwa kushinda mechi zote tatu

Alianza kwa kuwabamiza Chipukizi Fc mabao 3-1, kisha akawachapa Mtibwa sugar mabao 2-0 kabla ya kutinga fainali kibabe kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo Fc

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’