Simba imetumia michuano ya kombe la Mapinduzi kuwafanyia majaribio wachezaji watatu waliotoka nchi za Zimbabwe, Uganda/Sudan
Nyota hao ni beki wa kati Kelvin Moyo, kiungo mshambuliaji Ian Nyoni na beki mwingine wa kati Β Bernard Agele
Kwa wastani nyota hao ni wazuri lakini kwa hakika hawawazidi walinzi wazawa kina Ame Ibrahim na Kennedy Juma na hata viungo washambuliaji kina Ibrahim Ajib, Miraji Athumani na Hassan Dilunga
Kama uongozi wa Simba unafikiria kuwasajili nyota hawa ni bora wabaki na nyota waliopo wasubiri dirisha kubwa la usajili
Maoni ya mashabiki wengi wa Simba wameonyesha kutoridhishwa na viwango vya nyota hao kwa mlinganisho na wachezaji waliopo
ADVERTISE HERE