Okwi, Kwasi wakimbiza kwa mauzo ya jezi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Feb 2018
Okwi, Kwasi wakimbiza kwa mauzo ya jezi
Kulingana na uchunguzi uliofanywa na gazeti la NIPASHE, jezi ya beki mpya wa Simba, Asante Kwasi na mshambuliaji, Emmanuel Okwi, zimekuwa zikinunuliwa zaidi na mashabiki wa soka kuliko za wachezaji wengine wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Jonas Kisesa, mmoja wa wachuuzi wa jezi na vifaa vingine vya michezo aliliambia gazeti hilo kuwa jezi za wachezaji hao wawili ndio zinanunuliwa zaidi kila anapokuwa anafanya biashara hiyo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Kisesa alisema kuwa awali ilikuwa jezi ya Okwi na Ibrahim Ajib wa Yanga lakini sasa soko limebadilika na hiyo inatokana na wachezaji hao wanavyoonyesha kiwango kizuri katika mechi mbalimbali wanazocheza za ligi.

"Sasa hivi tunauza sana jezi ya Okwi na Asante Kwasi, ila hata za Tshishimbi (Papy) pia tunaziuza sana, naamini hadi mwisho wa msimu Simba ikiendelea kushinda na Okwi akifunga hakuna atakayemkamata, yaani hata picha yake inauzika sana," alisema muuzaji mwingine, Ally Hamad.

Kuhusu idadi ya mashabiki wanaoingia uwanjani, mechi za Simba zimekuwa zinaongoza kwa kuhudhuriwa na watazamaji wengi zaidi.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’