Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Suleiman Matola amesema malengo yake ni kuona kikosi chake kinatwaa taji la Michuano ya Mapinduzi na hilo litatimia kama watashinda mchezo wa leo wa nusu fainali dhidi ya Namungo Fc
Simba itachuana na Namungo Fc katika mchezo wa pili wa nusu fainali utakaopigwa kuanzia saa mbili na robo usiku
Mchezo wa kwanza ni kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc na utapigwa saa kumi Alasiri
Kuelekea mchezo wa Namungo, Matola amesema wachezaji wako kwenye hali nzuri isipokuwa Pascal Wawa na Mohammed Hussein ambao watasubiri ripoti ya daktari kama wataweza kutumika leo
Nyota wengine watakaokosekana ni Luis Miquissone aliyebaki jijini Dar es salaam baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Platinum Fc
Fundi Clatous Chama yeye alipewa ruhusa kurejea kwao Zambia kushughulikia matatizo ya kifamilia