Aliyekuwa kocha wa Simba Patrick Aussems amesema yuko tayari kurejea Msimbazi kuchukua nafasi ya Sven Vandenbroeck huku akitamba kuwa kikosi cha sasa Simba kinaweza kutisha kimataifa kama kikitumika vizuri.
Sven amesema kwa ubora wa kikosi cha Simba, ana uhakika anaweza kuifikia rekodi yake ya kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
"Nipo tayari kurudi tena kuifundisha timu hiyo kwani imekuwa na kikosi bora zaidi ya misimu miwili nyuma wakati nawafundisha. Nipo tayari kurudi kama nitapokea simu kutoka kwa kiongozi wa Simba, lakini wakati huu nipo katika tafakari ya maamuzi kwani nina ofa kutoka katika timu mbalimbali za huko Afrika," Aussems alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
"Kwa maana hiyo nipo tayari kurudi Simba kama watanifuata na milango ipo wazi kwani ni miongoni mwa timu ambayo falsafa yangu ya kucheza soka la kushambulia na kuvutia mashabiki na wachezaji wake wana sifa nyingi za kuelewa na kuutumia kwa haraka"
"Simba nimeishi nao vizuri na milango ipo wazi na nawapa nafasi kuliko timu nyingine yoyote ambayo inanihitaji. Simu ambayo nimepokea ni ya kiongozi mmoja mkubwa kutoka Azam kuona namna gani naweza kuja huko ila hatukufika mbali na hatukuendelea zaidi katika maongezi haya," alisema Sven
Simba bado iko kwenye mchakato wa kusaka mbadala wa Sven Vandenbroeck aliyeondoka juzi kujiunga na klabu ya FAR Rabat ya nchini Morocco