Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema wameendelea kupokea maombi ya makocha mbalimbali wanaotaka kurithi nafasi iliyoachwa na Sven Vandenbroeck aliyetimkia Morocco kujiunga na FAR Rabat
Mpaka kufikia jana, Simba ilipokea maombi ya makocha zaidi ya 100 wanaotaka kuinoa klabu ya Simba
Barbara amesema watakuwa makini katika uchambuzi wao ili kuhakikisha wanampata kocha bora atakayekidhi vigezo walivyoweka
"Tangu kuandoka kwa Sven tayari tumepokea wasifu (CV), kutokea nchi mbalimbali Afrika na Ulaya wote wameomba kazi ya kuja kuifundisha timu yetu naimani ambaye tutamleta ni yule mwenye uwezo mkubwa na hatachukua muda wa kuendeleza timu.
"Jambo la kuondoka kwa Sven ni la muda mfupi, lakini Simba haijabadilisha wachezaji bali ameondoka kocha na ambaye tutamleta ni yule mwenye uwezo na mchakato tayari umeanza haraka katika orodha hiyo naimani tutampata ambaye tunamuhitaji," alisea Barbara
Simba inahitaji kumpata kocha mpya haraka ili kwendana na ratiba ya michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi, mechi zikitarajiwa kuanza kupigwa mwezi ujao