Mkude hawezi kukwepa lawama

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Feb 2018
Mkude hawezi kukwepa lawama
Kiungo Jonas Mkude hakuwemo kwenye kikosi cha Simba kilicholazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mwadui FC juzi.

Inaelezwa kuwa Mkude alichelewa uwanja wa ndege hivyo kuachwa jijini Dar es salaam wakati Simba ilipoondoka kuelekea Shinyanga.

Baadae alisafiri kuungana na wenzake mkoani humo.

Tukio hilo linadaiwa kumkera kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre pamoja na benchi lote la ufundi hivyo kuamua kumuweka nje kwenye mchezo huo.

Pengo la Mkude aliye katika kiwango bora sana lilikuwa dhahiri na ndio sababu mashabiki wengi wa Simba wamemshushia lawama.

Japo sababu ya kuchelewa kwake ndege haijawekwa wazi, lakini ni dhahiri sababu hiyo haikulishawishi benchi la ufundi na ndio maana 'aliadhibiwa' kwa kuachwa nje ya kikosi.

Kocha Lechantre amekuwa akisisitiza nidhamu kwa wachezaji wake huku akiwataka waweke mbele maslahi ya timu.

Mkude ni mchezaji kipenzi cha mashabiki wa Simba, uwezo wake dimbani sio wa kutiliwa shaka.

Lakini ni muhimu sana ahakikishe mafanikio yake kama mchezaji hayaathiriwa na masuala ya nutovu wa nidhamu.

Kwani mwisho wa siku hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu ya Simba.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’