Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chipukizi hapo jana, michuano ya kombe la Mapinduzi inaendelea leo Simba ikitarajiwa kushuka tena dimbani kuikabili Mtibwa Sugar
Mchezo huo utakaopigwa saa mbili na robo usiku, ni kumbukumbu ya mchezo wa fainali mwaka jana, Mtibwa Sugar ikishinda bao 1-0
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Selemani Matola amesema leo wamedhamiria kulipa kisasi dhidi ya wakatamiwa hao
Matola amesifu kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake kwenye mchezo wa jana, Simba ikitokea nyuma dhidi ya Chipukizi Fc na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1
ADVERTISE HERE