Simba imeshinda mchezo wa kwanza kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar baada ya kuichapa Chipukizi Fc mabao 3-1
Bao la Meddie Kagere na mabao mawili yaliyowekwa kambani na Miraji Athumani yameihakikishia Simba kuondoka na ushindi huo muhimu ambao hakuna shaka umewasogeza karibu na nusu fainali ya michuano hiyo
Vijana wa Chipukizi walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 37 kabla ya Kagere kusawazisha kwenye dakika ya 44
Kipindi cha pili Simba ikadhihirisha kuwa wao ni wakubwa sana mbele ya Chipukizi kwa mabao mawili ya Sheva
Aidha Miraji ameibuka kuwa nyota wa mchezo huo akiondoka na kitita cha Tsh 200,000/-
Simba itakamilisha mchezo wa pili kesho dhidi ya Mtibwa Sugar
ADVERTISE HERE