Usiku wa kuamkia leo uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuachana na kocha Sven Vandenbroeck kwa makubaliano ya pande mbili
Taarifa za Sven kuachana na Simba zilianza kusambaa jana jioni kocha huyo akiwa tayari ameondoka nchini
Kocha Msaidizi Selemani Matola anatarajiwa kuiongoza timu katika kipindi ambacho watakuwa wakisaka kocha mpya
Simba imemtakia Sven kila la kheri huko aendako
Akiwa na Simba Sven ameshinda mataji yote msimu uliopita pamoja na kuisaidia Simba kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu
Pia ameiacha Simba ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi
Nani atarithi mikoba yake? Tusubiri....
ADVERTISE HERE