Vifaa vipya kujaribiwa Mapinduzi Cup

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Jan 2021
Vifaa vipya kujaribiwa Mapinduzi Cup

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema kuwa, kabla ya dirisha la usajili kufungwa kuna jambo ambalo watalifanya kwa baadhi ya wachezaji wapya ambao watakuwa wanawahitaji katika kikosi

Pamoja na kuridhishwa na uimara wa kikosi cha Simba, Barbara amesema wanaweza kusajili, baadhi ya wachezaji wanaowahitaji wanaweza kuwajaribu katika michuano ya kombe la Mapinduzi

"Kwa sasa ukiangalia kikosi chetu ni kipana na kina wachezaji wazuri, sioni sababu ya kumsajili mwingine ila tunakwenda kucheza Kombe la Mapinduzi na kuna baadhi ya wachezaji watakuja kufanya majaribio"

"Kama watatufurahisha kidogo labda tunaweza kubadilisha mawazo. Wachezaji hao watatoka katika maeneo mbalimbali na kuna ambalo tutaangalia ni mahitaji ya timu ambayo kama itatokea kati ya hao waliokuja kufanya majaribio amekidhi tutamsajili ili kuzidi kuimarisha timu yetu kuwa bora katika mashindano yote," alisema Barbara

Lwanga amepona

Katika hatua nyingine, Barbara amesema kiungo mkabaji Thaddeo Lwanga anaweza kuanza kuonekana kikosini katika michuano ya kombe la Mapinduzi

Mtendaji huyo wa Simba amesema walipata ITC ya Lwanga mapema lakini hakuwa tayari kuanza kucheza baada ya kupata majeraha

"Taddeo alikuwa anakosekana uwanjani kwa kuwa alikuwa ni mgonjwa, lakini matibabu yake yamekwenda vizuri na wapenzi pamoja na mashabiki ambao wamekuwa wakimuulizia mara kwa mara wataanza kumuona katika Kombe la Mapinduzi"

"Kuhusu vibali vya kazi na vingine vyote kama ITC tayari tumeshavipata na tumekamilisha kila kitu na kazi imebaki kuona namna gani tunaweza kumtumia katika mashindano yote ambayo yapo mbele yetu"

Kikosi cha Simba tayari kimewasili visiwani Zanzibar kesho Ijumaa wakitarajiwa kushuka kwenye uwanja wa Amaan kuikabili Chipukizi Fc

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’