Sven amejibu maswali ya wengi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Jan 2021
Sven amejibu maswali ya wengi

Wakati mwingine ni vyema kuwaamini makocha kwani wanafahamu maamuzi wanayoyachukua ili kuhakikisha timu inapata mafanikio

Mashabiki huwa tunakuwa na wachezaji wetu tunaowapenda na tunapendelea kuwaona uwanjani kila wakati timu inapocheza

Lakini Kocha Sven Vandenbroeck amekuwa tofauti na msimamo wa wengi wetu

Sven amesimamia katika kile anachokiamini na kamwe hakubadili chochote sababu ya kelele zetu mashabiki

Jana amepata alama nyingi sana baada ya kuiwezesha Simba kutinga hatua ya makundi kibabe michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Ushindi wa mabao 4-0 umepatikana uwanja wa Benjamin Mkapa huku Sven akitumia timu yake anayoiamini yeye ambayo kwa kiasi kikubwa siyo waliyokuwa wakiitarajia mashabiki

Wakati akimkosa Jonas Mkude, Mbelgiji huyo akafanya mabadiliko mengine kwa kuwaanzisha Larry Bwalya na Said Ndemla eneo la kiungo huku akiwaacha nje nahodha John Bocco na Meddie Kagere

Kuanza na walinzi watatu nyuma kuliwezesha Simba kuwa bora sana katika kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni, Shomari Kapombe na Luis Miquissone wakin'gara zaidi wakitokea pembeni

Kwa hakika leo Sven alikuwa shujaa wa Simba kimbinu, nadhani ifike wakati mashabiki tuache kujivika utaalam tusiokuwa nao

Naamini Sven anakwenda kufanya vizuri zaidi kwenye hatua ya makundi ukilinganisha na mtangulizi wake Patrick Aussems

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’