Kwa mara nyingine Simba imedhihirisha kuwa wao ni miamba wa soka Tanzania, Afrika Mashariki na pengine hata kusini mwa Jangwa la Sahara baada ya leo kuifumua Platinum Fc mabao 4-0 na kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Simba inaenda makundi kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu
Mabingwa wa nchi waliingia katika mchezo huo wakiwa na lengo moja tu, kusaka ushindi muhimu, walianza kulisakama lango la Platinum tangu dakika ya kwanza
Lakini walihitaji dakika 39 kuhesabu bao la kwanza kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Erasto Nyoni baada ya Shomari Kapombe kuvutwa shati ndani ya eneo la hatari
Wababe hao wa soka nchini walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo moja
Kipindi cha pili ilikuwa Simba iliyoendelea kutakata na katika dakika ya 61 Kapombe aliyekuwa bora sana, akamalizia kimiani mpira uliotemwa na mlinda lango wa Platinum baada ya shuti la Larry Bwalya
Kuna mwamba wa Lusaka mmoja, Clatous Chama kwani ndiye aliyeihakikishia Simba ushindi mnono na kuipeleka makundi kwa mara ya pili

Baada ya kuwatoka walinzi wa Platinum, Chama alimwachia Larry Bwalya aliyemsetia Bocco kuweka kambani bao la tatu kabla Chama mwenyewe hajaweka kambani bao la nne kupitia mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya eneo la hatari
Vita imemalizika jijini Dar es salaam, Simba imeibuka washindi wa vita hiyo na sasa tunaelekea hatua ya makundi kupambana na wababe wenzetu barani Afrika
Bravooooo Mnyaamaaaaa...!