Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji amesema Watanzania wote wanapaswa kuiombea Simba iweze kufanya vizuri kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc kwani ushindi wa Simba utakuwa na faida kwa nchi
Mo amesema Simba ikishinda na kutinga hatua ya makundi, itakuwa imeitangaza Tanzania lakini pia wataongeza nafasi ya timu zitakazoshiriki michuano ya CAF
"Tuombe kheri Simba iweze kufanya vizuri, inapofanya vizuri sio tu faida kwetu bali nafasi ya kuweza kupeperusha bendera ya Tanzania na kuongeza nafasi za ushiriki katika mashindano ya kimataifa," amesema Mo
Simba itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa Jumatano saa 11 jioni kuikabili Fc Platinum katika mchezo ambao mabingwa hao wa nchi watahitaji ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili kuweza kutinga makundi