Uongozi wa klabu ya Simba umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo wakati itakaposhuka kwenye dimba la Benjamin Mkapa kucheza dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika kesho Jumatano
Katika mchezo huo, Simba wanahitaji ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza jijini Harare, Zimbabwe dhidi ya FC Platinum Desemba 23 mwaka jana
Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema mipango ya maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo yamekamilika, lakini kubwa zaidi wanahitaji kuona mashabiki wao wanajitokeza kuwapa ari siku hiyo ya mchezo
Mchezo huo awali ulipangwa kuanza saa 1:00 usiku, utafanyika kwenye uwanja huo kuanzia saa 11:00 jioni ili kuwapa nafasi mashaiki wengi kujitokeza kuwashangilia.
"Tulituma ombi kwa Caf kuomba ratiba ya mchezo irudishwe nyuma na wamekubali, lengo la kufanya hivyo ni kutoa fursa kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kwakuwa ni muda ambao utawanufaisha wengi baada ya kutoka kazini" alisema Manara katika Mkutano na Wanahabari jana
Aidha, manara aliongeza kuwa wameliomba Shirikisho la Soka Afrika, Caf, kuingiza mashabiki kwa asilimia 100 baada ya shirikisho hilo kutaka mashabiki waingie nusu ya idadi inayoingizwa na uwanja husika. Bado wanasubiri jibu hilo ili wauze tiketi 60,000
Simba ilifanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa jana, leo watakuwa kwenye uwanja wao wa Mo Simba Arena kukamilisha maandalizi ya mwisho
Platinum Fc iliyowasili nchini mwishoni mwa wiki iliuyopita, leo itafanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kauli mbiu ya mabingwa wa nchi Simba kuelekea mchezo huo ni War In Dar (WIDAR), Fc Platinum lazima 'wapasuke' hapo kwa Mkapa kuhakikisha Simba inakwenda makundi