Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki kuhakikisha wanakuwa na tiketi zao mapema tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumatano uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza na Wanahabari mapema leo katika Mkutano uliofanyika Serena Hotel, Manara amesema muda wa mchezo ni saa 11 jioni
Manara amesema mafanikio iliyopata Simba katika michuano iliyopita yalitokana na ushirikiano mkubwa waliopata kutoka kwa mashabiki wao

"Hatujawahi kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote bila ya nguvu ya mashabiki, Simba sisi sio klabu ya wazalendo wala Wananchi ila ni watu, hii sio klabu ya Haji Manara hii sio Chama, sio Bocco sio nani"
"Mashabiki wanatakiwa kuimba War In Dar, hawatoki Wazimbabwe. Tumefanya hivyo kwa Al Ahly, Nkana, hata AS Vita," alisema Manara
Aidha, Manara amewataka mashabiki wasioitabia mema Simba katika mchezo huo wabakie nyumbani kwani kwenda uwanjani ni kujitafutia maradhi tu, Simba imedhamiria kushinda mchezo huo na kutinga hatua ya makundi
"Huna sababu ya kuwashangilia Fc Platinum bora ubaki nyumbani umejifunika gubigubi kwasababu Simba baada ya saa 11 tutakuwa tumeshafuzu. Tena ni bora sisi tuvuke hatua hii maana tukitoka tutakuja kuchukua Ubingwa wa VPL back to back na nyie mkaendelea kupanda Kimbinyiko"