Kikosi cha Simba kinakamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Fc Platinum ambao utapigwa keshokutwa Jumatano uwanja wa Benjamin Mkapa
Kurejea kwa mshambuliaji Chris Mugalu kumeongeza mzuka kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu ya Simba
Nahodha John Bocco amekuwa nje kwa wiki kadhaa akisumbuliwa na majeraha ambapo kocha Sven Vandenbroeck amesema hatma yake ya kucheza mchezo huo itategemea na hali yake ya afya katika siku mbili za mazoezi ya mwisho
Viungo Mzamiru Yassin na Thadeo Lwanga nao wanaweza kukosekana kwenye mchezo huo kutokana na majeraha
Simba imeshapokea ITC ya Lwanga lakini nyota huyo wa Kimataifa wa Uganda alipata majeraha wakati Simba ikijiandaa na mechi dhidi ya Majimaji na Ihefu Fc
Jumatano Simba itakuwa ikisaka ushindi wa kuanzia mabao 2-0 dhidi ya Platinum Fc ili kujihakikishia kutinga hatua ya makundi
Platinum Fc waliwasili nchini juzi tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni