Ni wazi kiungo Said Khamis Ndemla atapewa majukumu ya dimba la kati kwenye mchezo dhidi ya Platinum Fc ambao utapigwa Jumatano, Januari 06, uwanja wa Benjamin Mkapa
Ndemla ameaminiwa na kocha Sven Vandenbroeck akifanya vizuri katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Majimaji na Ihefu Fc
Wapo walioingia hofu baada ya uongozi wa Simba kumsimamisha Jonas Mkude kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu
Lakini ni wazi Ndemla anaweza kuwa mbadala wake, hakuna shaka atamudu majukumu kwenye eneo la kiungo
Bado uongozi wa Simba unahaha kupata kibali cha kiungo Thaddeo Lwanga ambaye bado chama cha soka Misri hakijaweza kuiachia ITC yake licha ya Simba kukamilisha taratibu zote
Lwanga bado hajacheza mechi yoyote tangu ajiunge na Simba wiki chache zilizopita, ITC ikitajwa kuwa sababu