Kamati ya Nidhamu ya klabu ya Simba inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili shauri la kiungo Jonas Mkude ambaye amesimamishwa kutokana na tuhuma za utovu wa Nidhamu
Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amewataka wapenzi, wanachama, mashabiki wa klabu ya Simba pamoja na wanahabari kuwa watulivu
"Suala la Mkude litatolewa ufafanuzi wiki ijayo baada ya kamati husika kuketi. Tunawaomba wanachama na mashabiki wetu kuwa watulivu wakati tukisubiri kamati ifanye kazi yake," alisema Barbara
Kumekuwa na presha kubwa kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakitaka shauri la Mkude lisikilizwe mapema ili kiungo huyo mahiri awe sehemu ya kikosi kitakachoikabili Fc Platinum Januari 06
ADVERTISE HERE