Hans Poppe atuliza mashabiki Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
17 Feb 2018
Hans Poppe atuliza mashabiki Simba
Baada ya Simba kulazimishwa sare 2-2 na Mwadui, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo Zacharia Hanspope amewatuliza mashabiki na kuwaambia washushe presha kwani kikosi chao cha msimu huu kiko sasa na ubingwa ni lazima.

Mashabiki wa Simba waliondoka kimya kimya uwanjani baada ya Paul Nonga kuisawazishia Mwadui bao la pili dakika ya 89.

Pamoja na matokeo hayo Simba imeendelea kukaa kileleni kwa pointi 42 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 37, jambo linalowapa presha mashabiki wa timu hiyo.

Akizungumza baada ya mchezo huo Hanspope alisema wala sare hiyo isiwape presha mashabiki kwani msimu huu ubingwa ni wao.

“Unajua msimu huu tuna timu bora sana kwani tumesajili wachezaji wenye kiwango cha juu kwa hiyo tusiwe na presha ya ubingwa kabisa na hii sare isitupe wasiwasi”alisema Hanspope kwa kujiamini.

Alisema sasa wanakwenda kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Africa dhidi ya Gendarmarie Nationale ya Djibout.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →