Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwapa furaha mashabiki wao katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ihefu Fc
Mchezo huo ni wa kwanza duru ya pili, mabingwa hao watetezi wakishinda kwa mabao 2-1 mchezo wa kwanza uliopigwa mkoani Mbeya
Aidha huu ni mchezo wa mwisho kufunga mwaka 2020, Machampioni wamepania kufunga mwaka kibabe kwa kuondoka na ushindi mnono
Kocha Sven Vandenbroeck amesema atautumia mchezo huo kuwa sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc ambao utapigwa wiki ijayo
Simba inahitaji kushinda leo ili kuendelea kulinda nafasi ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne mfululizo
Leo Wanamsimbazi watarajie kukiona kile kikosi cha mauaji kitakachosheheni nyota wote tayari kugawa dozi ya funga mwaka
mchezo utaunguruma kuanzia saa kumi kamili jioni