Nahodha wa Simba John Bocco amerejea mazoezini kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc utakaopigwa Januri 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya KMC yalipelekea Bocco akose mchezo wa kwanza kule Zimbabwe, mchezo ambao Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0
Mfungaji bora huyo wa muda wote ligi kuu ya Vodacom, juzi pia alikosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Majimaji
Kocha Sven Vandenbroeck anaweza kumpumzisha kesho kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu Fc kumuweka sawa kwa ajili ya kumaliza kazi Januari 06
ADVERTISE HERE