Baadhi ya vyombo vya habari ni kama vina ajenda ya siri na Simba kwa kuibua masuala ambayo hayana ukweli wowote
Mwezi uliopita Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' aliweka bayana kuwa suala la usajili wa kiungo Clatous Chama alishalimaliza
Mwamba wa Lusaka akikubali kuongeza mkataba wa miaka miwili utakaomuweka Msimbazi mpaka mwaka 2023
Kaimu Mwenyekiti wa Simba Mwina Kaduguda akaongeza kuwa Mo alitua zaidi ya Tsh Milioni 700 kumbakisha Chama Msimbazi kutokana na umuhimu wake kikosini
Taarifa ya Mo na Mwenyekiti ndio taarifa sahihi na ya mwisho kabisa kuaminiwa na Wanamsimbazi
Wanasimba wameaswa wasiamini sana yanayoripotiwa na baadhi ya magazeti kwani ni dhahiri wana ajenda zao ziwe za kibiashara au kutaka kuwavuruga tu Wanamsimbazi
Simba ilishafunga mjadala wa usajili wa Chama kwa kumuongeza mkataba wa miaka miwili