Nisemeni mimi, waacheni wachezaji wangu - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Dec 2020
Nisemeni mimi, waacheni wachezaji wangu - Sven

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameeleza kutofurahishwa na ukosoaji unaoelekezwa kwa wachezaji wake katika michezo iliyopita ya ligi ya mabingwa

Akizungumza jana baada ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Majimaji ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0, Sven amesema wachezaji wake wanajitoa kwa hali na mali kuhakikisha timu inafanya vizuri, hivyo hafurahii kuona wanalaumiwa pasipo sababu za msingi

"Tangu mchezo wa kule Nigeria, tumekuwa na changamoto ya ugonjwa lakini wachezaji wangu wameendelea kuipigania timu bila ya kujali hali zao. Naomba vyombo vya habari, mashabiki iwe ndani au nje ya klabu ya Simba muwaache wachezaji hawa, nizungumzieni mimi"

"Wachezaji wanajitoa sana kwa moyo mmoja kuipigania timu. Tukishinda moja, mbili au tatu naomba mnilaumu mimi. Mnilaumu kwa mavazi ninayovaa au kama nahitaji kukata nywele zangu. Nawaomba muwaache wachezaji wangu," alisema Sven kwa uchungu

Aidha akizungumzia mchezo dhidi ya Majimaji, Sven ameeleza kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake

"Tulifanya mabadiliko ya kikosi cha zaidi ya asilimia 90, nawapongeza wachezaji wangu kwani tangu dakika ya kwanza walionyesha kuwa na shauku ya kupata matokeo"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’