Mwadui FC ikiwa katika dimba lake la nyumbani imefanikiwa kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Vodacom, Simba.
Bao la kusawazisha lililofungwa na Paul Nonga kwenye dakika ya 89 limemaliza mwenendo wa Simba kutopoteza pointi katika michezo saba iliyopita.
Aidha mlinda lango Aishi Manula amefungwa kwa mara ya kwanza mwaka huu. Alikuwa hajaruhusu mpira kutinga katika nyavu zake tangu mwezi Novemba mwaka jana.
Nahodha wa Simba John Bocco alianza kuifungia timu yake bao la kuongoza kwenye dakika ya tisa akipachika bao safi la kichwa kufuatia mpira wa faulo uliopigwa na Shiza Kichuya
Bocco aliumia kwenye dakika ya 29 na nafasi yake kuchukuliwa na Laudirt Mavugo.
Mwadui FC wakasawazisha kwenye dakika ya 59 mfungaji akiwa David Luhende kupitia mpira wa adhabu.
Simba ikicheza kwa tahadhari kubwa ugenini ilipata mkwaju wa penati katika dakika ya 68 baada ya mlinzi wa Mwadui FC Mgeveke kumuangusha Okwi ndani ya eneo la hatari.
Okwi alifunga mkwaju huo wa penalti na kuihesabia Simba bao la pili pia likiwa bao lake la 14.
Simba ilipata pigo kwenye dakika ya 84 baada ya mlinzi Juuko Murshidi kutolewa nje kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Nonga akainusuru Mwadui FC na kipigo kwenye dakika za majeruhi.
Matokeo hayo yanaendelea kuibakisha Simba kileleni kwa tofauti ya alama tano baada ya kufikisha alama 42.d
Yanga iko nafasi ya pili ikiwa na alama 37.

ADVERTISE HERE