Simba imeanza kampeni ya kutetea ubingwa wa kombe la FA kibabe baada ya kuishushia kipigo cha mabao 5-0 Majimaji katika mchezo wa raundi ya tatu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Wakiwa katika kiwango bora sana, vijana wa Sven Vandenbroeck walihitaji dakika mbili tu kuanza kuhesabu mabao kupitia kwa mlinzi wa kushoto Gadiel Michael
Gadiel alimalizia mpira uliokuwa umetemwa na mlinda lango wa Majimaji baada ya shuti la Said Khamis Ndemla
Wakiendelea kulisakama lango la Majimaji, mabingwa hao wa kandanda nchini walifunga bao la pili kupitia kwa Chris Mugalu aliyemalizia pasi murua iliyochongwa na Francis Kahata
Simba ilienda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0, kipindi cha pili wakaendeleza pale walipoishia kwa mabao ya Ibrahim Ame, Meddie Kagere na Luis Miquissone
Ushindi ni matokeo yaliyowapa furaha mashabiki wa Simba, mabingwa hao wa nchi wakitinga kibabe raundi ya nne ya michuano hiyo
Sven alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake akiwapa nafasi wachezaji ambao wamekuwa hawachezi mara kwa mara
Kwa hakika leo hawakumuangusha mbelgiji huyo kwani nyota hao walikuwa na kasi na ari kubwa ya kuhakikisha Simba inaondoka na ushindi