Leo ni kumbukumu ya siku ya kuzaliwa mshambuliaji wa Simba Miraji Athumani 'Sheva'
Sheva alianza vyema maisha yake kwenye klabu ya Simba msimu uliopita alipojiunga akitokea klabu ya Lipuli Fc
Majeraha aliyopata mwanzoni mwa msimu uliopita yalimpunguza kasi na amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kocha Sven Vandenbroeck
Miraji bado ni moja ya wachezaji wanaohitajika kwenye kikosi cha Simba, amedhihirisha hilo kila alipopewa nafasi
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii muhimu ya kumbukumbu kwake
Bila shaka leo atasherehekea Birthday vyema kwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Majimaji katika mchezo wa raundi ya tatu kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Happy Birthday Sheva...!
ADVERTISE HERE