Baada ya shamrashamra za sikukuu ya Krismasi kumalizika, leo burudani inarejea kwa Wanamsimbazi wakati mabingwa wa Taifa hili Simba watakaposhuka uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na Majimaji katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) raundi ya tatu
Simba ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo na wamedhamiria kuendelea kulishikilia taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo
Mabingwa hao wa soka nchini wanarejea kwenye mikiki mikiki ya mashindano ya ndani baada ya kukamilisha mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc ambao ulipigwa mapema wiki hii nchini Zimbabwe na wenyeji kushinda bao 1-0
Wazimbabwe hao watakuja nchini wiki ijayo kwa ajili ya mchezo wa marudiano
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck anafahamu leo vijana wake wanahitaji ushindi wa mabao mengi ili kupandisha morali ya kikosi chake
Mchezo utapigwa kuanzia saa moja kamili usiku