Yanga wanajisumbua kwa Morrison - Rage

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Dec 2020
Yanga wanajisumbua kwa Morrison - Rage

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amefunguka kuwa Yanga kuendelea kung'ang'ania suala la Morrison kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ni sawa na kupoteza muda kwani hakuna chochote ambacho watapata kwenye kesi hiyo.

Rage alikwenda mbali kwa kusema kuwa hakuna sheria yoyote inayosema mshitaki na mshitakiwa wote wanatakiwa kulipia fedha ili kesi yao iweze kusikilizwa na CAS kama ambavyo taarifa ya Yanga ilivyosema wao na Morrison wanatakiwa kuchangia fedha za Kifaransa 'Franc' 24,000 kwa maana ya kila mmoja kuchangia Franc 12,000

"Kama kweli wametumiwa hiyo barua na CAS ya kulipia hizo fedha waambie wakuonyeshe hizo karatasi, hakuna kitu kama hicho kwamba mshitakiwa na mshitaki wanatakiwa kulipa ada ya kesi yao kusikilizwa"

"Wanachofanya Yanga ni kupoteza muda tu, hawatapata chochote. Nikwambie kuwa kesi zote za CAS zitasikilizwa Januari 12, chukua maneno yangu kesi zote zilizopo CAS zitasikilizwa na hakutakuwa na kesi ya Morrison na Yanga," Rage amenukuliwa na gazeti la Championi

Juzi klabu ya Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Frederick Mwakalebela alisema kuwa wametumiwa barua na CAS wakitaarifiwa kuwa Jaji wa kusikiliza shauri lao la kimkataba na Morrison amepatikana na watatakiwa kulipia kiasi hicho cha fedha kabla ya Januari 12, mwakani ili kesi iweze kusikilizwa.

Yanga walikata rufaa na shauri lao kulipeleka CAS mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kubaini upungufu kadhaa kwenye mkataba wa Morrison ambao alipewa na Yanga, na hadi wakati kesi yake ikiendelea tayari alikuwa amesaini Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’