Coastal Union wamtaka Ame kwa mkopo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Dec 2020
Coastal Union wamtaka Ame kwa mkopo

Klabu ya Coastal Union imetuma maombi kwa klabu ya Simba wakimuhitaji beki Ibrahim Ame kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu

Ame alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu akitokea klabu ya Coastal Union akiunda ukuta mahiri na Bakari Nondo ambaye alisajiliwa na Yanga

Kocha wa Coastal Union Juma Mgunda amesema anahitaji kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo msimu huu imeruhusu mabao mengi

Simba inatajwa kuwa kwenye mkakati wa kuimarisha safu yake ya ulinzi, Ame anaweza kuruhusiwa kwenda kuwatumikia waajiri wake hao wa zamani

Mabosi wa Simba wanatarajiwa kuweka hadharani majina ya wachezaji wanaotolewa kwa mkopo

Mapema wiki hii Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez alieleza kuwa wako katika hatua za mwisho kumalizana na timu zinazowahitaji wachezaji wao kwa mkopo

Wachezaji ambao wamekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza ndio baadhi yao watatolewa kwa mkopo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
57m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’